ISRAEL imeendeleza na mashambulizi yake ya makombora kwenye eneo la kusini la mji mkuu wa Lebanon, Beirut, mapema leo likiwemo eneo lililo karibu na uwanja wa ndege wa pekee wa kimataifa wa Lebanon.

Israel iliendeleza na mashambulizi yake ya makombora kwenye eneo la kusini la mji mkuu wa Lebanon, Beirut, mapema leo likiwemo eneo lililo karibu na uwanja wa ndege wa pekee wa kimataifa wa Lebanon.

Jeshi la Israel lilikuwa limetoa notisi ya watu kuondoka katika eneo hilo, likidai kulikuwa na vifaa vya wanamgambo wa Hezbollah katika eneo hilo.Hizbullah yasema inaunga mkono usitishaji vita Lebanon

Kiongozi wa Hezbollah, Naim Kassem, katika hotuba yake ya kuadhimisha siku 40 tangu kuuwawa mtangulizi wake, Hassan Nasrallah, hapo jana, alisema kundi hilo liko tayari kwa mazungumzo ya usitishwaji wa mapigano ila iwapo tu, Israel itasitisha kile alichokiita uchokozi wake.

Haya yanafanyika wakati ambapo Israel ilitangaza kutanua operesheni yake ya ardhini kaskazini mwa Gaza na sasa itajumuisha sehemu ya mji wa Beit Lahiya, mji ambao umeshambuliwa pakubwa tangu siku za kwanza za vita hivyo.Hezbollah yavurumisha makombora dhidi ya Israel

Wakati huo huo, maelfu ya watu wameendelea kuandamana huko Israel kwa siku ya pili mfululizo wakipinga kuachishwa kazi kwa aliyekuwa Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant ambaye Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu alisema kwamba amepoteza imani naye.