Na Isri Mohamed
Mchezaji Simon Msuva amejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa (Taifa Stars) kitakachoingia kambini kesho Novemba 07, kujiandaa na mechi mbili za mwisho za kufuzu AFCON dhidi ya Guinea na Ethiopia.
Msuva alizua taharuki baada ya jina lake kukosekana kwenye listi ya wachezaji waliotwa kucheza dhidi ya DR Congo na Ethiopia, ambapo miongoni mwa waliotoa maoni yao juu yake ni mshambuliaji wa Congo, Fiston Mayele.
Akitangaza kikosi leo, Kocha Mkuu wa Stars, Hemed Morocco amesema kitu kikubwa anachoangalia ni kiwango cha wachezaji ambapo awali Msuva hakuwa na timu ndio maana hakuweza kumuita.
Aidha Kocha Morocco ameelezea sababu za kumuita Aishi Manula ambaye hajacheza mechi za kimashindano kwa muda mrefu ndani ya klabu yake ya Simba, na si Ally Salim ambaye ndiye aliyepata nafasi ya kucheza mechi nyingi zikiwemo za kimataifa akiwa na Simba.
“Ally namuheshimu sana amefanya kazi kubwa katika mechi alizocheza na ameweza kuhimili, lakini kwa mujibu wa walivyo kwenye klabu zao hakuna tofauti kubwa kati ya Aishi na Ally, kwa wakati huu nataka uzoefu Zaidi”
“Manula ni mchezaji mwenye zuoefu wa kutosha na amefanya vizuri katika mechi hizi mbili alizocheza, tutakuwa na wiki moja ya mazoezi, tutajaribu kufanya kila linalowezekana kuhakikisha anarudi katika kiwango chake”