Wakati zoezi la kupiga kura za Urais nchini Marekani, Mgombea Donald Trump wa chama cha Republican amejitangaza mwenyewe kama mshindi, kufuatia matokeo yanayoonesha kuwa kuwa yuko mbele kumzidi mpinzani wake Kamala Harris.
Trump ametangaza kushinda tena Urais wa Taifa hilo kwa asilimia 51.2% ya kura dhidi ya 47.4 % za Kamala Harris na hivyo kuwa Rais wa 47 wa nchi hiyo huku akitarajia kurejea tena katika Ikulu ya White House.
Hadi hivi sasa Trump amefikisha Kura za Wajumbe (Electoral Votes) 267 kati ya 270 zinazotakiwa, huku Kamala akiwa na Kura 224.
Kwa upande wa Kura za Wananchi Trump ana 68,654,143 huku mpinzani wake Kamala ana 63,558,470.