Na Lookman Miraji

Wizara ya michezo imesaini mkataba na kampuni ya ujenzi ya Suma JKT juu ukarabati wa viwanja vya michezo nchini.

Mkataba huo umesainiwa leo hii huko ikihusisha ukarabati ya viwanja vya michezo ambavyo vitatumika katika mashindano yajayo ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN) yatakayofanyika mapema mwakani 2025 pamoja na yale ya mataifa ya Afrika (AFCON) yatakayofanyika mwaka 2027 huku Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi mwenyeji.

Akizungumza leo wakati wa hafla hiyo Katibu mkuu wa wizara ya utamaduni, sanaa na michezo, Gerson Msigwa amesema kuwa wamechagua kuwapa tenda hiyo kampuni ya Suma JKT kwa kuwa wametambua wanauwezo wa kufanya kazi hiyo kwa kasi inayotakiwa kwani muda ni mfupi na kazi hiyo inahitajika kufanyika kwa kimkakati ili iweze kukamilika ndani ya muda.

“Tumechagua kuipa kazi hii kampuni ya SUMA JKT kwasababu tunafahamu wanauwezo wa kufanya kazi usiku na mchana kwasababu muda ni mfupi na tunahitaji kuifanya hii kazi kwa oparesheni ili iweze kukamilika ndani ya muda”

Aidha Katibu mkuu Msigwa ameongeza kuwa tayari serikali imetenga kiasi cha shilingi billioni 8 katika hatua za mwanzoni kukamilisha mchakato huo.

“Katika kutekeleza mchakato huu mheshimiwa Rais ameshatoa fedha, zaidi ya shillingi billioni 8 za kuanzia ili kazi hii ianze haraka iwezekanavyo ili ikamilike kwa ndani ya muda husika kuepukana na kupokwa uenyeji wa mashindano.”

“Tayari tumekamilisha kwa asilimia kubwa ujenzi wa viwanja baadhi ikiwemo Benjamin Mkapa ambao tunaelekea katika hatua za mwisho kabisa. Lakini kazi inaendelea katika ujenzi wa uwanja mpya jijini Arusha ambao ujenzi wake unaenda kwa kasi na umefikia katika asilimia 7 ambapo atatakiwa kutukabidhi uwanja mwezi Aprili 2026” Amesema.

Kwa upande mwingine pia Mkurugenzi wa kampuni ya Suma JKT, Morgan Nyoni nae ameeleza kuwa wako tayari kufanya kazi hiyo usiku na mchana kuhakikisha wanakamilisha kazi hiyo ndani ya muda uliopangwa.

“Tuko tayari kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha tunakabidhi kazi hii kwa wakati huku tukiwa tumeshaanza ujenzi wa viwanja baadhi na vingine tukiwa mbioni kuanza matengenezo”

Ukarabati wa huo wa viwanja vya vitahusisha viwanja vitano vya michezo jijini Dar es salaam ambavyo ni uwanja wa Meja Jenerali Isamuyo, kiwanja cha leaders(Kinondoni), Kiwanja cha farasi (Oysterbay), kuwa cha Gymkhana pamoja na kiwanja cha Losco.