Na Magrethy Katengu,JamhuriMedia
Dar es Salaam

Serikali imesema itaendelea kuthamini taaluma ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji majenzi kwa kuwapatia tenda za miradi zinazojitokeza ili wasivunjike moyo waendelee kuwa wazalendo na nchi yao.

Hayo yamesemwa na Oktoba 29,2024 Jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Wilaya ya Ilala ,Edward Mpogolo aliyemwakilisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt.Dotto Mashaka Biteko katika Mkutano wa tano wa Bodi ya wabunifu majengo na Wakadiriaji Majengo na hafla ya ugawaji vyeti kwa wahitimu uliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC)

” Tazama tulipotoka utagundua kuwa tumetoka mbali hivyo nikiri kuwa taaluma hizi ni muhimu sana na hatuna budi kuwashawishi wanafunzi wetu kupenda kusoma masomo ya Sayansi ili nchi yetu iendelee kujengeka” amesema DC Mpogolo

DC amesema wataalamu wa ndani ni budi kuchangamkia fursa za tenda za miradi zinazojitokeza ikiwezekana waungane siyo kutafuta wageni na kutegemea kupata asilimia ndogo kutoka kwao.

DC Mpogolo amesema baadhi ya wataalamu wa ubunifu wa Majengo na ukadiriaji Majenzi wamekua wakiangalia maisha yao binafsi kwa ajili ya kujipatia fedha za muda mfupi huku suala la weledi kazini likiwa limewekwa pembeni hali ambayo inasababisha majengo kuwa chini ya kiwango na kutoendelea kuaminika .

Sanjari na hayo serikali ipo kwenye mchakato wa kufanyia maboresho sera ya ujenzi ili kutengeneza Sheria ya ujenzi itakayosidia wataalamu hao kufikia matamanio ya kukuza sekta ya ujenzi kutokana na mabadiliko ya teknolojia yanayoenda kwa kasi Duniani.

“Jitihada zinazopatikana katika sekta ya ujenzi inatokana na nyinyi wataalamu wa ubunifu wa Majengo na ukadiriaji Majenzi,ukiona mafanikio yaliyopo kwa sasa yanatokana na nyinyi,nyinyi nawaomba sana muwe Wazalendo ili tumuunge mkono Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan” amesema DC Mpogolo.

Kwa upande wake mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Dkt Daudi Kondoro ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania( TBA) amesema kuwa watendaji wa Wizara wataendelea kusimamisha sekta ya wataalamu wa ubunifu wa Majengo na Wakadiriaji Majenzi ili waweze kua na weledi katika kazi zao.

“Wizara ya ujenzi itatenga fedha kwa ajili ya kuendelea kutoa mafunzo wataalamu 180 Kila Mwaka ambao wanahusika na bunifu wa Majengo na ukadiriaji Majenzi,ili waweze kujengewa weledi zaidi na zaidi katika taaluma yao” amesema Dkt.Kondoro.

Na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi wa wabunifu wa Majengo na Wakadiriaji majenzi (AQRB) Dkt Ludigija Bulamile amesema kuwa kwa sasa Bodi hiyo imesajili 1586 ambapo kati yao 33 ni wageni kutoka nje ya nchi hivyo shughuli zao wanazozifanya zinakwenda kwa kuzingatia weledi na wale wanaokosea wamekuwa wakiwaonya ili wasitie doa wazawa kutoaminika

Naye Miongoni mwa aliyetunukiwa cheti Mhandisi Alfayo Khamisi ameshukuru sana kufikia hatua hiyo hadi kupata cheti hivyo atajitahidi anakwenda kuwajibika katika shughulizake kwa weledi.