Waandishi wa habari watatu wameuawa katika shambulizi la anga la Israel dhidi ya jengo linalojulikana kuwa na wanahabari kusini-mashariki mwa Lebanon, walioshuhudia wameiambia BBC.
Shambulio hilo lilitekelezwa kwenye nyumba ya wageni inayotumiwa na waandishi wa habari katika eneo la Hasbaya inayotumiwa na waandishi wa habari zaidi ya kumi na wawili kutoka angalau mashirika saba ya habari – na ina ua wa kuegeshwa magari yaliyowekwa alama “vyombo vya habari”.
Waandishi wa habari watatu wa kiume walikuwa wakifanya kazi katika vituo vya utangazaji vya Al-Manar TV na Al Mayadeen TV, ambavyo vilitoa taarifa kuhusu namna walivyowaenzi wafanyakazi wao waliouawa.
Waziri wa habari wa Lebanon amesema shambulio hilo lilifanywa kimakusudi na kulitaja kuwa ni uhalifu wa kivita.
Jeshi la Israel bado halijatoa maoni yoyote, lakini awali lilikanusha kuwalenga waandishi wa habari.