Na Magrethy Katengu,JamuhuriMedia,
Dar es Salaam
Jumuiya ya Afika Mashariki EAC imesema itahakikisha inaweka mikakati ya kupambana na uhalifu uliovuka mipaka ikiwemo usafirishaji binadamu,dawa za kulevya,ugaidi na hualifu wa mitandao .
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP leo Oktoba 25,2024 Mkurugenzi Upelelezi Makosa ya Jinai Kamishna DCI Ramadhani Kingai katika mkutano wa 8 ulifanyika Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na nchi 6 Wakuu wa Polisi kutoka nchi sita Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC .
Sambamba na hayo amesema Tanzania ni moja ya nchi inayoshirikiana na nchi nyingine ili kuweza kusaidia ardhi ya Afrika Mashariki inakuwa salama ambapo mpaka sasa wamekuwa wakibadilishana taarifa za wahalifu kupitia mtandao na wengine wamekamatwa na kuweza kudhibitiwa.
” Jumuiya yetu ni budi kuimarisha miundombinu ya usalama na kubadilishana taarifa kwani tunatambua changaomto kubwa Uhalifu wa mitandaoni na Vishiria vya ugaidi ndiyo shida inayotusumbua hivyo nchi moja haiwezi peke yake kulabiliana lazima kuwepo na mashirikiano na mikakati ya pamoja’ amesema DCI Kingai.
Kwa upande wake Kaimu Mpelelezi aliyemwakilisha Mkuu wa Polisi Sudani Kusini Thomasi Thomasi amesema mkutano huo ni mahusihusi unakwenda kujadili sera za pamoja kuweza kukabiliana na uhalifu ili kusaidia Usalama wa bara la Afrika.