Na Magrethy Katengu,JamuhuriMedia,
Dar es Salaam

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema litachukua tahadhari zote za kiusalama kabla, wakati na baada ya mchezo Usalama utakuwa wa kiwango cha juu siku ya mchezo wa mpira wa miguu kati ya Simba na Yanga katika maeneo yanayozunguka uwanja ,ndani, nje na barabara za kuingia nakutoka uwanjani.

Akizungumza leo Oktoba 18 jijini Dar es Salaam Kamanda Jeshi la Polisi Kanda Maalum SACP Jumanne Muliro amesema Jeshi linafuatiia kwa karibu sana mchezo wa soka utakaochezwa Jumamosi tarehe 19 Oktoba 2024 kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam kwani Mchezo.wa watani wa jadi kati ya klabu ya utachezwa kuanzia saa 11:00.

“Onyo hairuhisiwi mtu yeyote kwenda uwanjani na silaha ya aina yoyote, isipokuwa baadhi ya askari wenye jukumu la usalama eneo hilo,pia magari yatakayo ruhusiwa kuingia uwanjani ni yale yenye kibali maalum” amesema Kamanda

Aidha Jeshi laPolisi inatoa wito kwa wapenda michezo kuendeea kuwa wastaarabu na kujiepusha na vitendo vya aibu kabla, wakati na baada ya mchezo huo. Jeshi la Polisi inawatakia kila la kheri timu zote mbili na matokeo yoyote yatakayotokea ya mchezo huo wayakubali

Please follow and like us:
Pin Share