Na Isri Mohamed

BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imemtangaza mwamuzi Ramadhan Kayoko kutoka Dar es Salaam kuwa refa atakayesimamia sheria 17 za mchezo wa soka kwenye Derby ya Kariakoo itakayopigwa Jumamosi, Oktoba 19, 2024 katika dimba la Benjamin Mkapa.

Akizungumza na wanahabari mapema leo, Afisa habari wa bodi ya ligi, Karim Boimanda amesema Kayoko atasaidiwa na Mohamed Mkono kutoka Tanga na Kassim Mpanga kutoka Dar es Salaam, huku mwamuzi wa akiba akiwa ni Tatu Malogo katika mchezo huo utakaopigwa kesho majira ya saa 11:00 jioni.

Kayoko ana historia ya kuchezesha Derby zaidi ya mara mbili, ambapo mara ya mwisho alichezesha Septemba 25, 2024, Yanga akimfunga Simba bao moja kwa Nunge.

Baada ya mechi hiyo Kayoko alibaki midomoni mwa watu kufuatia kitendo chakutoa kadi nyekundu kwa aliyekuwa kiungo wa Simba, Taddeo Lwanga na kadi 8 za njano kwa ujumla.

Simba ambaye ni mwenyeji wa mchezo huo ameshacheza mechi tano za ligi kuu mpaka sasa, anashika nafasi ya pili kwenye msimamo akiwa na pointi 13, Huku Yanga akiwa amecheza mechi nne, anashika nafasi ya nne na alama 12.

Please follow and like us:
Pin Share