Rais William Ruto amemteua Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki kuwa Naibu Rais ajaye kufuatia kutimuliwa kwa Rigathi Gachagua Alhamisi usiku.

Jina la Kindiki limewasilishwa bungeni ambapo wabunge wanatarajiwa kulipigia kura.

Spika Moses Wetang’ula alitangaza uteuzi huo katika Kikao maalum kilichoandaliwa Ijumaa.

Nimepokea ujumbe kutoka kwa rais kuhusu uteuzi wa Profesa Kithure Kindiki kujaza nafasi katika afisi ya Naibu Rais wa Jamhuri ya Kenya,” Wetang’ula alitangaza. Katiba inasema pindi rais anapowasilisha uteuzi kwenye Bunge, wabunge watapiga kura ya kulikataa au kuliidhinisha jina hilo. Pia hakuna sharti la kura ya thuluthi mbili.

“Prof. Kindiki, ambaye kwa sasa anahudumu kama Waziri wa Mambo ya Ndani na Utawala wa Kitaifa, atahitaji idhini kutoka kwa Bunge la Kitaifa kabla ya kushika nafasi ya Naibu Rais. Bunge lazima lipigie kura uteuzi ndani ya siku 60 baada ya kupokea jina hilo.

Baada ya kuidhinishwa, mteule atateuliwa rasmi na Rais kuwa naibu wake. Ingawa Katiba haijaweka bayana muda wa uteuzi huu, unatarajiwa kutokea mara baada ya kuidhinishwa na Bunge.

Katika maandalizi ya uchaguzi mkuu wa 2022, Kindiki alikuwa miongoni mwa waliopendekezwa kuwa mgombea mwenza wa Ruto lakini hatimaye akaamua kumchagua Gachagua.

Baadaye alielezea kwamba alimchagua Gachagua kwa sababu ya umri wake na alifikiri wangeelewana zaidi.

Mwanzoni mwa kuondolewa kwa Gachagua, kulikuwa na mazungumzo ya Kindiki kuwa ndiye anayefuata kuchukua nafasi yake.

Bunge la Seneti lilipiga kura ya kumtimua Naibu Rais Rigathi Gachagua kufuatia mchakato wa siku mbili uliohusisha ushahidi wa kina .

Gachagua aliondolewa baada ya Maseneta kuunga mkono sababu tano kati ya kumi na moja zilizowasilishwa na Mbunge wa kibwezi kaskazini Mwinge Mutuse.

Tunaendelea kukupasha…

Please follow and like us:
Pin Share