WAKILI Peter Madeleka ameiomba mahakama ya Wilaya ya Dodoma kumsomea mashtaka mtuhumiwa Afande Fatma Kigondo, ya kubaka kwa kundi, akiwa hospitalini alipolazwa akipatiwa matibabu.

Wakili Madeleka ameyasema hayo baada ya Wakili wa Afande Kigondo anayeitwa Sedric Mbunda kueleza kuwa mtuhumiwa ameshindwa kufika makamani Oktoba 07, kusikiliza kesi yake kwa sababu ni mgonjwa.

“Mheshimiwa Hakimu tunaiomba mahakama yako tukufu kusaini malalamiko haya tuliyowasilisha dhidi ya Fatma Kigondo ili yatumike kama hati ya mashtaka, na baada ya kusainiwa mshtakiwa asomewe mashtaka yake katika hospitali yoyote aliyopo bila kujali anaumwa ugonjwa gani, iwe Muhimbili, Benjamin Mkapa, Bugando au sehemu yoyote ili hatua zingine za kisheria ziendelee”

Baada ya maombi hayo wakili, Nyambuli Tungaraja aliahirisha kesi hiyo hadi Ijumaa Oktoba 17, atakapotoa maamuzi baada ya kupitia baadhi ya vifungu vya sheria.

Please follow and like us:
Pin Share