Mkuu wa Majeshi mstaafu, Jenerali Venance Mabeyo amemuelezea marehemu Meja Jenerali Mstaafu, Charles Mbuge kama miongoni mwa vijana wake watiifu ambao amewahi kufanya nao kazi.

Jenerali Mabeyo ameyasema hayo kwenye halfa ya kuuaga kijeshi mwili wa Mbuge iliyofanyika Lugalo jijini Dar es Salaam.

“Alikuwa ni mchapakazi na anayethamini kazi, kila akipewa jukumu lazima alitekeleze kwa nguvu zake zote, na hiyo ndio ilikuwa sifa yake kubwa, kwahiyo na sisi tujifunze kutoka kwake kutimiza wajibu wetu”

“Alikuwa ni mcheshi wakati wote, anapenda kuungana na kuzungumza na watu maneno mazuri, ya kujenga na yenye maendeleo zaidi, mimi nilimpenda alikuwa rafiki yangu, kijana wangu mtiifu na mtumishi mwenzangu, na tumechapa kazi vizuri”

Mwili wa Meja Jenerali Mstaafu Mbuge aliyefariki Oktoba 12, akiwa nchini India akipatiwa matibabu, tayari umefikishwa nyumbani kwao kijijini Nyamongo mkoani Mara kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Please follow and like us:
Pin Share