Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam

SERIKALI kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) itaendelea kuboresha huduma za upakuaji mafuta ili kupunguza muda wa meli kusubiri bandarini na hivyo kuboresha upatikanaji wa bidhaa hiyo kwa uhakika

Akizungumza Oktoba 16, Mhandisi wa Mradi wa Ujenzi wa Matenki ya Kuhifadhia na Kusambaza Mafuta Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam, Mhandisi Hamis Mbutu amesema mradi huo utahusisha ujenzi wa matenki 15 yenye jumla ya mita za ujazo 378,000.

Amesema kukamilika kwa mradi huo kutawezesha gharama za maisha kwa wananchi kurahisisha ufanyaji biashara pamoja na shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Kwa upande wake Ofisa Uhusiano TPA, Enock Bwigane amesma mradi huo umegharimu Sh bilioni 678.6

Meneja wa mradi huo, Liu Tau ameeleza kuwa watahakikisha mradi huo unakamilika ndani ya muda uliopangwa na hivyo kuweza kuwanufaisha wananchi wa Tanzania kwa ujumla.

Please follow and like us:
Pin Share