Onyo la Washington limetajwa kuwa lenye uzito zaidi tangu kuzuka kwa mapigano kati ya Israeli na wapiganaji wa Hamas mwaka uliopita.
Aidha onyo hilo pia limejiri baada ya Umoja wa Mataifa kufanya tathimini wikendi iliopita na kubaini kwamba hakuna misaada mipya ya kibinadamu imeingia katika Ukanda wa Gaza katika kipindi cha wiki mbili.Washington katika onyo lake imeitaka Israeli kuhakikisha kwamba misaada ya kutosha inawasilishwa katika Ukanda wa Gaza kuwasaidia raia walioathirika na mapigano katika kipindi cha siku 30.
Iwapo Israeli haitofanya hivyo, huenda ikapoteza msaada wa kijeshi wa mabilioni ya fedha kutoka kwa Marekani.Onyo la Marekani linakuja ikiwa imetimia mwaka mmoja tangu kutokea kwa mapigano katika Ukanda wa Gaza, makabiliano ambayo Rais Joe Biden wa Marekani amekuwa akiitaka Israeli kuhakikisha haiwadhuru raia wa kawaida wa Palestine.
Biden amekuwa miongoni mwa viongozi wa dunia wanaoiunga mkono Israeli tangu shambulio la Hamas la tarehe saba ya mwaka uliopita.