Na Lookman Miraji, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Naibu Waziri mkuu Dotto Biteko amezindua rasmi mkutano wa Afrika wa nishati.

Mkutano huo umezinduliwa rasmi leo hii jumatano ya oktoba 16 katika ukumbi wa hoteli ya kempiski, Dar es salaam.

Akizungumza hii alipofungua mkutano huo waziri Biteko ameeleza kuwa ni heshima kubwa kwa Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo kwani heshima hiyo imekuja kufuatia mahusiano mazuri ya kidiplomasia kati ya taifa la Tanzania, benki ya maendeleo ya Afrika pamoja na benki ya dunia.

“Ni heshima kwetu kuwa mwenyeji wa mkutano huu. Nchi yetu tumefanikiwa sana kwa siku za hivi karibuni ukilinganisha na nchi nyingine katika Usimamizi wa sekta ya nishati . Na hiyo ndio miongoni mwa sababu kubwa zaidi iliyoshawishi mkutano huu kufanyika nchini ikiwa pamoja na mahusiano mazuri kati ya Tanzania, benki ya Afrika na benki ya dunia.”

Waziri Biteko ameeleza kuwa lengo kuu la mkutano huo ni majadiliano juu ya mpango kazi uliowekwa na nchi za Afrika kuhakikisha mpaka kufikia mwaka 2030 zaidi ya watu millioni 30 barani Afrika wanafikiwa na umeme. Ambapo waziri Biteko amekiri kuwa ni kazi kubwa inayohitaji mipango thabiti kuhakikisha mpango huo unakamilika.

“Mkutano huu unafanyika ukiwa na lengo la kujadiliana kuona mipango gani ifanyike kuhakikisha tutakapofika mwaka 2030 watu zaidi ya millioni 300 barani Afrika wanafikiwa na umeme. Ni jambo ambalo ni kazi kubwa kwa miaka 5 inayokuja ya kuhakikisha watu hao wanapata umeme”

Aidha waziri huyo amegusia pia kuhusu dhamira ya serikali juu ya mchakato wake wa kuhakikisha mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka huu vijiji vyote nchini vinafikiwa na umeme ambapo zaidi ya vijiji elfu 12 vimelengwa na mpango huo.

Kwa upande mwingine pia benki ya maendeleo ya Afrika kupitia muwakilishi wake ambae pia ni Mkurugenzi wa benki kwa hapa nchini Bi: Patricia Laverley imesema kuwa benki hiyo inatambua na kuthamini jitihada kubwa zinazofanywa na wizara ya nishati hapa nchini katika kutatua changamoto za nishati zinazoikabili jamii ikiwa pia na uboreshwaji juu upatikanaji wa nishati.

Aidha mkurugenzi pia ameeleza kuwa wanaunga mkono jitihada za kukabiliana na nishati chafu ambapo kwa mujibu wa takwimu zinasema takribani asilimia 90 ya watanzania bado wanajihusisha na matumizi ya nishati ya mkaa hivyo wanashirikiana na serikali kuhakikisha mpaka kufikia mwaka 2030 wanafanya mageuzi kutoka katika matumizi ya nishati chafu kwenda katika dunia ya sasa ya matumizi ya nishati safi.

“Benki ya maendeleo ya Afrika tunatambua mchango mkubwa wa wizara ya nishati nchini Tanzania juu ya uboreshwaji kwenda katika malengo makuu ya upatikanaji na usambazwaji wa nishati safi.”

“Nchini Tanzania, inakadiriwa asilimia 90 ya Watanzania bado wanategemea nishati ya mkaa katika kupikia ambayo inachangia pakubwa changamoto ya afya na kuchochea ukatwaji wa miti ovyo. Tuko tayari kuwezesha jitihada za serikali katika kuchochea mabadiliko kutoka katika matumizi ya nishati chafu kwenda katika matumizi ya nishati safi mpaka kufikia mwaka 2030.” alisema.

Mkutano huo wa Afrika unategewa kuwa wao siku mbili ambapo utahitimika hapo kesho Oktoba 17, mwaka huu.

Please follow and like us:
Pin Share