Na Lookman Miraji,JamhuriMedia, Dar es Salaam

Ikiwa ni oktoba 14 ya mwaka 2024 ambapo taifa la Tanzania linaadhimisha miaka 25 tangu kufuatia kifo cha aliyekuwa baba wa taifa la Tanzania Hayati Julius Kambarage Nyerere.

Siku hiyo ambayo ni siku maalumu ya kumuenzi kiongozi huyo aliyekuwa anayetambulika kama muasisi wa taifa hilo huadhimishwa kila ifikapo tarehe 14 oktoba kila mwaka.

Hayati Julius Nyerere alizaliwa mnamo Aprili 13 mwaka 1922 huko mkoani butiama.

Rais Julius Nyerere enzi za uhai wake aliongoza jitihada za kupigania uhuru kwa taifa la Tanganyika mpaka kupatikana kwa uhuru wake mnamo mwaka 1961 kutoka katika utawala wa waingereza.

Julius Nyerere pia anatajwa kama miongoni mwa wanadiplomasia hodari na vigogo waliowahi kutokea katika historia ya bara la Afrika kufuatia jitihada zake za kuyasaidia baadhi ya mataifa ya Afrika katika ukombozi uhuru kutoka katika utawala kikoloni.

Taifa la Afrika Kusini kupitia balozi wake nchini Tanzania, Noluthando Mayende Malepe limetoa salamu juu ya maadhimisho ya sikukuu hiyo ya hayati Julius Nyerere.

Salamu hizo zimetolewa leo hii na Balozi Noluthando Mayende Malepe huku akizungumzia juu ya urafiki ulioko kati ya taifa la Tanzania na Afrika kusini ushirikiano ulioasisiwa na viongozi wakuu wa mataifa hayo wakiwemo hayati Nyerere na hayati Nelson Mandela.

Balozi Noluthando ameeleza kuwa anaungana na mamilioni ya watanzania katika kuadhimisha siku hiyo kwani taifa la Afrika Kusini linatambua mchango wa hayati Nyerere katika ukombozi uhuru wa taifa hilo na mataifa mengine yaliyoko ukanda wa kusini mwa bara la Afrika.

“Naungana na mamilioni ya watanzania kukumbuka na kuadhimisha urithi wa kiongozi huyu ambae ni ishara ya udongo wa Afrika. Mwalimu Julius Nyerere alitoa mchango mkubwa kwetu katika harakati za ukombozi na bara na Afrika hususani ukanda wa kusini mwa Afrika. Nchi za ukanda wa kusini mwa Afrika zikiwemo Msumbiji, Angola, Namibia na Zimbabwe zilinufaika vilivyo na mchango uliotolewa na hayati Nyerere wakati wa ukombozi wa uhuru wa mataifa yao. Tukirejea nyuma katika historia tunashukuru mchango mchango mkubwa tuliopewa na Tanzania kwetu juu mataifa haya ya kusini mwa Afrika kwani raia wake walijtolea kwa mioyo yao kuwa pamoja na wapigania uhuru wa mataifa.”

Balozi Noluthando aliongeza kwa kuzungumzia mahusiano makubwa ya kirafiki yaliyokowepo kati ya hayati Nyerere na hayati Nelson Mandela ambapo ameeleza kuwa ulikuwa ni urafiki mzuri kati ya waasisi hao wawili hali iliyopelekea mara baada ya hayati Mandela kutoka kifungoni na kuwa rais alilitembelea taifa la Tanzania ikiwa ni sehemu ya shukran alizozipata kutoka kwa viongozi taifa ambapo kubwa zaidi linalokumbukwa ni kupewa hati ya kusafiria yenye utambulisho wa kitanzania.

Aidha balozi Noluthando ameyataja mahusiano yalioko baina ya taifa la Afrika Kusini na Tanzania kuwa mahusiano bora endelevu katika nyanja mbalimbali zikiwemo kibiashara, uchumi pamoja na mabadilishano kati ya watu na watu huku akizihamasisha zaidi mahusiano ya kibiashara baina ya mataifa hayo mawili.

“Urafiki kati ya viongozi hawa wawili ulikuwa ni bora ambao unaashiria mahusiano mazuri ambayo mataifa haya yanayo kati nyanya za kibiashara , uchumi na hata mabadilishano kati ya watu na watu. Hivyo sisi ni marafiki tumekuwa pamoja katika nyakati mbalimbali hivyo ningependa kuona maendeleo zaidi na ningependa kuona kampuni kutoka nchini Afrika Kusini zikija kuwekeza nchini Tanzania na Zanzibar pia na kuona kampuni za kitanzania kwenda nchini Afrika Kusini kwa kwaajili ya kuwekeza na fursa za kibiashara kwa ujumla” Amesema.

Akiongeza balozi huyo amesema kuwa taifa la Afrika Kusini linajivunia hayati Nyerere kwani ni sehemu ya historia yao pia.

“Leo natamani kusema kwa watanzania kuwa hazina ya kumbukumbu kwa kiongozi huyu na kuhakikisha kuwa wanaadhimisha urithi ulioachwa kwao na kwetu pia. Sisi ni wenye shukran na wenye utambuzi wa uongozi jasiri ambao ulitolewa na viongozi wetu kama mwalimu Julius Nyerere ambao si kitu cha kawaida ila ni ukumbusho wa kutafakari juu ya mnyororo ambao tumesafiri na watanzania, tuko pamoja na watanzania sisi kama waafrika kusini” Amesema balozi Noluthando.

Please follow and like us:
Pin Share