Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry William Silaa (Mb) akizungumza jambo leo Oktoba 15, 2024 wakati akifungua  Kongamano la nane la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) linalofanyika kuanzia Oktoba  13 – 17, 2024 katika  Ukumbi wa Mikutano wa Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Bw. Mohammed  Abdulla akizungumza jambo leo Oktoba 15, 2024 katika ufungua  Kongamano la nane la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) linalofanyika kuanzia Oktoba  13 – 17, 2024 katika  Ukumbi wa Mikutano wa Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.

Picha za maukio mbalimbali Kongamano la nane la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

……………..

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema itaendelea kusimamia sera ya utekelezaji ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), kukuza utaalamu na uwekezaji, kujenga uwezo pamoja na kushirikiana na wadau mbalimbali kufanya utafiti.

Akizungumza leo Oktoba 15, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akifungua Kongamano la nane la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry William Silaa (Mb), amesema kuwa  Serikali imeendelea kuwekeza TEHAMA pamoja ya sheria ili kuifanyia Tanzania kuwa sehemu ya mabadiliko ya teknolojia Duniani.

Silaa amesema kuwa imeendelea kuwekeza katika TEHAMA ambayo imeonekana kuwa nguzo kuu ya kufikia Uchumi wa Kidijitali katika Nyanja mbalimbali Duniani.

“Hivi sasa dunia ipo katika kipindi cha Mapinduzi ya nne, tano sita ya viwanda ambapo shughuli za kiuchumi, kijamii na uzalishaji inakwenda kuendeshwa kwa kutumia teknolojia ” amesema Mhe. Silaa.

Mhe. Silaa amebainisha  kuwa Wizara imepewa jukumu la kusimamia sera ya TEHAMA 2016 ambayo inalenga kukuza matumizi ya TEHAMA nchini.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Bw. Mohammed  Abdulla, amesema kuwa lengo la Kongamano hilo ni kuwakutanisha wadau wa sekta ya TEHAMA kwa ajili ya kupata fusa ya kujadili masuala yanayohusu teknolijia  ili kuhamasisha matumizi yake nchini.

“Kongamano hili lina sura ya kimataifa ambapo washiriki kutoka ndani ya nchi na nje ya nchi wameshiriki, tutashuhudia utoaji wa tuzo ya Kimataifa na Tanzania imekuwa mwenyeji kwa kuwa nchi ya kwanza kufanyika mashindano haya yaliyoandaliwa na Umoja wa Afrika kuhusu masuala ya Akili Mnemba na Roboti” amesema Bw. Abdulla.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA, Prof. Leonard Msele amesema kuwa  Kongamano hilo limekuwa wakijadilia masula mbalimbali ya uchumi wa digitali lakini kwa mwaka huu wamejikita katika eneo la Akili Mnemba na Roboti kwa sababu ndio eneo linalojadilliwa zaidi Duniani.

Katika Kongamano la nane la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) limebeba kauli mbinu isemayo : Kutumia uwezo wa Akili Mnemba na Roboti kwa mapinduzi ya kiuchumi na kijamii.

Please follow and like us:
Pin Share