Na Egbart Rwegasira, JamhuriMedia, Misenyi

Halmashauri ya Wilaya Misseny mkoani Kagera Kupitia kwa mkurugenzi mtendaji wa Wilaya hiyo John Paul Wanga imetoa kiasi cha shilingi milioni moja ili kusaidia Matibabu ya Betson Mjuni Bernard (03).

Mtoto huyo Mwenye umri wa miaka mitatu mzaliwa wa Kata Kitobo mkoani Kagera, alipata tatizo la jicho na mwanzoni mwa mwezi wa saba mwaka huu ilimlazimu kufanyiwa upasuaji mkubwa katika hosptali ya Taifa ya Muhimbili ambapo alipona kisha kuruhusiwa kurudi Nlnyumbani.

Mwanzoni mwa mwezi Oktoba mtoto huyo alianza kuviba tena jambo lililofanya wazazi wa mtoto huyo kuanza utaratibu wa kutafuta pesa ya kurudi tena hosptali ya Taifa Muhibili, ambapo Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo wakili John Paul wanga alimuagiza Mganga Mkuu wa wilaya kuratibu utaratibu wa haraka ili kuhakikisha mtoto huyo anasafirishwa kuelekea Hospital ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi.

Jamhuri Digitaqa tumefanya Mawasiliano na mama mzazi wa mtoto, na amesema ” Nashukuru nimepata kusaidiwa tayari taratibu zote zimefanyika na jioni hii naanza safari kuelekea jijini Dar es Salaam “

Kwa upende wake Mkurugenzi John Paul wanga amesema, Lengo la Mheshimiwa Raisi Samia Suruhu Hassani Ni kuhakikisha Wananchi wanasaidiwa pale inapoonekana mkono wa serikaliunahitajika , na kama mteule wa Raisi jukumu Lake kubwa ni kuhakikisha anabeba maono ya kiongozi wake.

Please follow and like us:
Pin Share