Na isri Mohamed

Uongozi wa klabu ya Coastal union umewajulisha rasmi mashabiki na wadau kwamba timu hiyo itautumia Uwanja wa Sheikh Amri Abedi, Arusha kama uwanja wake wa nyumbani kwa michezo yake inayofuata.

Taarifa iliyotolewa na ‘Wanamangush’ leo Oktoba 10, 2024 imebainisha kuwa uamuzi wa kupeleka mechi Jijini Arusha umezingatia mambo mengi sana yakiwemo kuthamini pendekezo la wanachama na wapenzi wa klabu hiyo.

Mambo mengine yaliyozingatiwa ni kuibakisha timu katika Kanda ya kaskazini, kuthamini kazi kubwa anayofanya mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ya kuinyanua Kanda ya kaskazini kupitia Jiji la Arusha, ombi la muda mrefu la Wana Arusha na uhakika wa kupata alama 3.

“Tunawaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kuendelea kuipa sapoti timu yetu nguvu na ari ile ile. Hata sasa kazi kwenu Wana Arusha timu Bora kutoka ukanda wenu hiyo.” imesema Coastal Union.

Please follow and like us:
Pin Share