Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Tabora

MAKAMU wa Rais Dkt. Philip Mpango amempa rungu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, kuwashughulikia wanaohujumu tumbaku mkoani Tabora.

Hatua hiyo imekuja baada ya waziri huyo kuwatolea uvivu wanaohujumu kilimo cha tumbaku na kumueleza Makamu wa Rais kuwa jopo hilo linaongozwa na qafanyabiashara watumishi, wanasiasa na vingozi wa vyama vya ushirika.

Akizungumza jana katika mwendelezo wa ziara yake ya siku nne mkoani Tabora Makamu wa Rais Dkt. Mpango amempa rungu Waziri Bashe kutowaonea haya wahusika na kuendelea kuwachukulia hatua.

“Mimi na Rais Dkt. Samia tunakupa ridhaa Waziri wa Kilimo washughulikie na chukua hatua tupo nyuma yako, hatuwezi kuvumilia watu wanaohujumu sekta hii muhimu ya kilimo cha tumbaku.

“Kampuni zisizo taka kulipa wakulima kwa wakati pia Waziri wafutie tu leseni usirudi nyuma waone haya kuwanyonya wakulima wetu,”amesema.

Makamu Mpango, amemuelekeza Waziri Bashe, kuendelea kushughulikia changamoto zilizopo katika masuala ya ruzuku kwa wakulima wa tumbaku kwani serikali haitaki kurudi nyuma.

Naye Waziri Bashe, amesema Uyui ni wakulima wazuri wa tumbaku na mpunga, tatizo kubwa lililopo sekta ya tumbaku ni hujuma zinazoongozwa na wafanyabiashara watumishi, wanasiasa na vingozi wa vyama vya ushirika.

“Ninawajua na baadhi ni rafiki zangu genge hili lina nia ya kuua sekta ya tumbaku wakiongozwa na Ushirika, siwezi kuwavumilia sitasita kufuta vyama hivi na kuwataja hadharani mnaoshirikiana.

“Waliua tumbaku Tabora huko nyuma na wanataka kurudia sitakuwa tayari kushirikiki dhambi hii, vyama vikuu vya ushirika mjue fedha za ruzuku ya mkulima sio zenu msizipangie matumizi ya posho nimezuia bilioni 13 hizi hazitalipwa katika vyama zitalipwa moja kwa moja kwa wakulima,”amesema.

Ameongeza kuwa, anasikitika kuona Meneja wa chama cha Wetco amekuwa akiwapotosha wabunge hivyo anamuagiza Mrajisi Mkuu wa Vyama vya Ushirika kumchukulia hatua kwa kuongea uongo huku akijua ruzuku imekuja tangu mwezi wa 9.

“Wakulima msidanganywe maslahi yenu yatalindwa na serikali ruzuku ipo nimeagiza nataka orodha jina la mkulima, chama cha msingi idadi na akaunti yake tutalipa moja kwa moja kwa wakulima,”amesema.

Pia amemtaka Mkuu wa mkoa, kuhakikisha kampuni ya vodcel ambayo haijamaliza malipo kwa vyama viwili vya ushirika kukamilisha malipo hayo ndani ya siku saba la sivyo wafutiwe leseni na kushikiria dhamana.

Please follow and like us:
Pin Share