Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk Emmanuel Nchimbi amesema Serikali inayoongozwa na CCM ilianzisha stakabadhi ghalani kwa makusudi ili kuwalinda wakulima dhidi ya unyonyaji na hivyo kuboresha uchumi wa wakulima na wa nchi.


Alisema mfumo huo ulianzishwa kwa kuzingatia maelekezo ya chama kupitia ilani ya uchaguzi. Dk Nchimbi alisema kabla ya kuanzishwa kwa mfumo huo, wakulima wengi nchini walikuwa wakinyonywa kwa kuuza mazao yao chini ya bei halisi ya soko-hali iliyochangia umaskini wao.

Dk Nchimbi alikuwa akitoa ufafanuzi kuhusu umuhimu wa mfumo huo baada ya Mbunge wa Kisesa (CCM), Luhaga Mpina kudai kuwa mfumo huo mpya umevuruga bei ya mazao.


Dk Nchimbi aliwaambia wakazi wa Kata ya Mwandoya Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu kuwa mfumo huo ulianzishwa ili kuwalinda wakulima na kuwahakikishia malipo ya uhakika.

Please follow and like us:
Pin Share