📌 Lengo ni kutangaza fursa za uwekezaji kwenye Mafuta, Gesi Asilia na Nishati Mbadala

Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga ameshiriki Jukwa la Mawaziri (Ministerial Symposium) nchini Afrika Kusini ikiwa ni sehemu Kongamano la Wiki ya Mafuta Afrika (Afrika Oil Week) linalofanyika Jijini Cape Town.

Jukwaa hilo pia limehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Dkt. James Mataragio, Kamishina wa Petroli na Gesi Ndg. Goodluck Shirima na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli ( PURA), Mha. Charles Sangweni.

Maudhui ya Kongamano hilo ni pamoja na kutangaza fursa za uwekezaji katika miradi ya Mafuta, Gesi Asilia na Nishati Mbadala katika Bara la Afrika.

Kongamano hilo litamalizika tarehe 10, Oktoba, 2024 nchini humo.

Please follow and like us:
Pin Share