Watu wasiopungua 70 wameuawa na wengine wapatao 6,300 wamekimbia makaazi yao kufuatia shambulio lililofanywa katikati mwa Haiti na genge la wahalifu.

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limesema katika ripoti yao iliyotolewa wiki iliyopita kuwa, karibu asilimia 90 ya watu waliokimbia makaazi yao wanaishi na jamaa zao wengine huku asilimia 12 wakipata hifadhi katika maeneo mengine ikiwemo shule.

Shambulio hilo lilifanyika mapema siku ya Alhamisi katika eneo la Pont-Sonde huku maelfu ya watu wakilazimika kuyakimbia makaazi yao.

Msemaji wa tume ya maridhiano Bertide Harace amesema miili ya watu kadhaa ilikuwa imetapakaa mitaani huku wengi wakiuawa kwa kupigwa riasi ya kichwa.

Waziri Mkuu Garry Conille ameapa kuwa mkono wa sheria utawaandama wahalifu wote waliohusika na mauaji hayo.

Please follow and like us:
Pin Share