Vyombo vya habari vimeripoti kutokea kwa mashambulizi manne ya anga yaliyofanywa na Israel katika eneo la kusini mwa mji wa Beirut, muda mfupi baada ya Jeshi la Israel kuwahimiza watu waondoke katika ngome za Hezbollah.

Shirika la habari la kitaifa NNA limeripoti mashambulizi mawili katika maeneo ya kusini, kwanza likilenga eneo la Saint Therese na lengine likitokea katika eneo la Burj al-Barajneh.

NNA imeyaeleza mashambulizi hayo kuwa “makali.” Mwandishi wa shirika la habari la AFP amesema madirisha yake yalitetemeka baada ya mashambulizi hayo huku mwengine akieleza kusikia milipuko mikubwa.

Taarifa ya jeshi la Israel imesema jeshi la IDF limeshambulia ngome za Hezbollah ikiwemo maghala ya silaha mjini Beirut.

Please follow and like us:
Pin Share