Vyombo vya habari vya serikali ya Lebanon vimesema mashambulizi matatu ya anga ya Israel yameipiga ngome ya Hezbollah kusini mwa Beirut siku ya leo.

Chanzo kilicho karibu na kundi hilo kimeliambia shirika la habari la AFP kwamba shambulio hilo lililenga jengo la ofisi ya uhusiano wa vyombo vya habari ya Hezbollah,” ambayo tayari “imehamishwa”.

Wiki hii, Israel ilitangaza kwamba wanajeshi wake wameanza “mashambulio ya ardhini” katika maeneo ya kusini mwa Lebanon ambayo yanaaminika kuwa ni ngome ya Hezbollah baada ya siku kadhaa za mashambulizi makali ya mabomu katika maeneo yote nchini gumo ambako kundi hilo la wanamgambo linayashikilia.

Baada ya takriban mwaka mmoja wa mapigano makali ya mpakani, Israel imehamisha mwelekeo wa operesheni yake kutoka Gaza hadi Lebanon, ambapo mashambulizi makubwa ya mabomu yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 1,000 na kuwalazimisha mamia kwa maelfu kukimbia.

Please follow and like us:
Pin Share