Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un leo ametishia kutumia silaha za nyuklia na kuisambaratisha kabisa Korea Kusini iwapo nchi hiyo itamchokoza.

Haya ni kulingana na taarifa iliyotolewa na vyombo vya habari nchini humo. Hii ni baada ya kiongozi wa Korea Kusini kuuonya utawala wa Kim kwamba utaangushwa iwapo atathubutu kutumia zana za nyuklia. Kim ametoa kauli hiyo wakati alipofanya ziara katika kitengo cha operesheni maalum cha jeshi.

“Iwapo Korea Kusini itajaribu kutumia jeshi kuingilia uhuru wa Korea Kaskazini, hali kama hiyo ikitokea, Seoul na Jamhuri ya Korea zitaangamia,” alisema Kim.

Majibizano kama hayo baina ya mataifa hayo mawili si jambo geni ila yanafanyika wakati ambapo kuna uhasama mkubwa baina ya mataifa hayo kutokana na hatua ya Korea Kaskazini hivi majuzi kufichua kwamba ina kinu cha nyuklia na hatua yake ya kuendelea kufanyia majaribio makombora.

Please follow and like us:
Pin Share