Na Dotto Kwilasa,JamhuriMedia,Dodoma

BENKI Kuu ya Tanzania (BOT)imeendelea kupiga marufuku watoa huduma mbalimbali nchini kufanya malipo ya ndani ya nchi kwa kutumia fedha za kigeni ambapo imesema kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Uamuzi huo unatokana na matarajio ya mfumuko wa bei kuendelea kuwa chini ya lengo la nchi la asilimia 5.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania,Emmanuel Tutuba ameeleza hayo leo Oktoba 3,2024 jijini hapa wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu taarifa ya Kamati ya ya sera ya fedha (MPC) ambapo alisema Bodi ya wakurugenzi wa Benki kuu Tanzania iliyokutana Oktoba 2,2024 imeamua Riba ya Benki Kuu (CBR) kuendelea kuwa asilimia 6
kwa robo mwaka itakayoishia Disemba 2024.

Mbali na hayo ametoa angalizo kwa watumiaji wa fedha hizo kuendelee kutumika tu pale ambapo mtu anafanya miamala inayovuka mipaka ni miamala kwenda nchi za nje hapo utakuwa umefanya biashara ya kimataifa na hapo ndipo unaporuhusiwa kutumia fedha za kigeni .

Tutuba ametoa rai kwa watanzania wote kutumia shilingi za Tanzania kufanya malipo na huduma za bidhaa ndani ya nchi na kwenye sheria nakutamka kwamba mtu atakayefanya malipo kwa kutumia fedha za kigeni ,anapofanya malipo ya ndani ya nchi kwa kutumia fedha za kigeni atakuwa ametenda kosa.

“Matakwa ya kisheria ambayo tunaendelea kusisitiza hususani kwa kufanya malipo ya ndani kwa kutumia shilingi ya Tanzania nayo yanaendelea kupunguza mahitaji ya fedha za kigeni hapa nchini na kuongeza ufanisi wa sera ya fedha,Niendelee kutoa wito wa kuendelea kuzingatia sheria kama mnavyokumbuka wakati wa bajeti Waziri wa fedha wakati anasoma bajeti na wakati wa kupitisha sheria ya fedha mwaka huu,”amesisitiza

Ameongeza,”Serikali na Bunge waliliridhia kwamba tuendelee kusimamia sheria ambapo kifungu cha 26 cha sheria ya Benki kuu kinatamka kwamba benki kuu itachapisha fedha itakayoitwa shilingi ya Tanzania fedha hiyo ndiyo itakayokuwa fedha pekee hali kwa malipo yote ya ndani ya nchi, “amesema

Tutuba ameeleza kuwa mtu anapofanya malipo ya bidhaa na huduma kwa kutumia shughuli za kitanzania lakini akatumia fedha za kigeni maana yake anafanya kosa ambalo kisheria na anastahili kupewa adhabu .

“Kwahiyo niendelee kuomba Benki na watanzania wote kwa ujumla unaponunua bidhaa ndani ya nchi tutumie shilingi ya Tanzania kwasababu kufanya hivyo ndiyo tunaendelea kusapoti sera ya fedha,wanatoa huduma mbalimbali za ada,wanaofanya malipo wanatoa risiti na wengine wanashawishi na kutoa invoice kwa kutumia fedha za kigeni kwa shughuli ambazo zipo ndani ya nchi wamefanya kosa ni waase waache kufanya hivyo, “amesema.

Aidha amesema benki kuu itaendelea kuimarisha akiba ya fedha za kigeni kupitia mpango wa ununuzi wa dhahabu katika soko la ndani kwa kutumia shilingi ya Tanzania na kwamba Upatikanaji wa fedha za kigeni unatarajiwa kuendelea kuimarika, kutokana na
ongezeko la bei ya dhahabu kwenye soko la dunia, shughuli za utalii na mauzo ya
bidhaa asilia kama korosho, tumbaku, kahawa na pamba.

Please follow and like us:
Pin Share