Na Isri Mohamed

Mahakama nchini Argentina imetoa ruhusa kwa mabaki ya Mwanasoka Nguli wa zamani Diego Maradona (aliyefariki mwaka 2020 kwa matatizo ya Moyo), kuhamishwa.

Mapema mwaka jana watoto hao waliomba mabaki ya Baba yao yahamishwe kutoka eneo la Makaburi binafsi na kupelekwa eneo la umma.

Watoto hao walieleza kuwa baba yao alikua mtu wa watu na ingekuwa vyema kama angezikwa sehemu ambayo watu wote wanaotaka wangepata nafasi kutembelea.

Aidha, Mahakama hiyo imesema kuwa watoto hao wataamua lini uhamisho huo ufanyike.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa eneo atakalohamishiwa lipo Puerto Madero jijini Buenos Aires na kwa sasa ujenzi wa eneo unaendelea.

Wakati huo huo watu 8 wakiwemo Madaktari na wauguzi wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani kujibu mashtaka ya kusababisha kifo cha Maradona.

Please follow and like us:
Pin Share