Na Isri Mohamed

Jeshi la polisi mkoani Njombe limekanusha kuwepo kwa matukio ya utekaji wa watoto mkoani humo kama ilivyoripotiwa na moja ya chombo cha habari.

Akizungumza na wanahabari kamanda wa polisi mkoani Njombe, ACP Mahamoud Banga amesema taarifa hiyo ina lengo la kupotosha umma kwani hakuna tukio lolote la utekaji watoto lililoripotiwa katika mkoa wao.

ACP Banga amesema wanaendelea kushirikiana na wazazi, walimu pamoja na Raia katika kupashana habari na kuzuia matukio ya kihalifu.

Aidha ametoa wito kwa vyombo vya habari kuwasiliana na makamanda wa polisi kwa ajili ya kupata ufafanuzi kabla hawajarusha ama kutoa taarifa ambazo zinaweza kuzua taharuki kwa wananchi.

Please follow and like us:
Pin Share