Uganda inasaka ufadhili wa ujenzi wa mitambo mitatu ya kuzalisha umeme wa nyongeza wa maji wa zaidi ya megawati 1,600, kwa lengo la kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya nishati hiyo.

Afisa wa Wizara ya Nishati nchini Uganda, Julius Namusaga, alitaja maeneo matatu muhimu yaliyoko kwenye Mto Nile, ambako mitambo hiyo inaweza kujengwa, na mkubwa zaidi ukiwa ni wa Ayago utakaozalisha megawati 840.

Miradi mingine inayolengwa ni mtambo wa Kiba utakaozalisha megawati 400 na Oriang, megawati 392, na kufanya uzalishaji kufikia megawati 3,678 sawa na asilimia 80 ya uzalishaji wa sasa.

Hivi sasa, karibu asilimia 85 ya umeme wa Uganda unazalishwa na vituo vya umeme wa maji, na uliosalia unazalishwa na mitambo ya joto na jua.

Please follow and like us:
Pin Share