Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limefanya kikao cha dharura usiku wa kuamkia Alhamis kujadili mzozo unaozidi kutanuka wa Mashariki ya Kati.

Balozi wa Iran kwa Umoja wa Mataifa ameliambia baraza hilo kwamba madhumuni ya nchi yake kuvurumisha makombora karibu 200 Israel ni kwa ajili ya kuizuia Israel kutoendelea na mashambulizi yake.

Wakati huo huo balozi wa Israel katika Umoja huo wa Mataifa Danny Danon amesema hatua hiyo ya Iran kuishambulia Israel ni kitendo kikubwa cha uchokozi na iwapo Iran haitozuiliwa basi wimbi jengine la makombora halitoilenga tu Israel bali mataifa mengine pia.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameapa kulipiza kisasikutokana na mashambulizi hayo ya Iran ila Iran nayo imejibu kupitia Rais Masoud Pezeshkian ikitishia kwamba itajibu vikali zaidi iwapo Israel itathubutu kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi.

Rais wa Marekani Joe Biden hapo Jumatano alisema kuwa hatoiunga mkono Israel iwapo itashambulia miundombinu ya zana za nyuklia za Iran.

Please follow and like us:
Pin Share