Wau wawili wameuwawa kwa kunyongwa na kamba kisha kutobolewa macho nyumbani kwao katika eneo la barabara ya nne jijini Tanga, huku baba mwenye nyumba Alii Mohamed Bagidad (60) hajulikani alipo.

Watu hao wamefahamika kama Saira Ali Mohammed (50) ambaye ni mama mwenye nyumba pamoja na binti wa kazi aliyetambulika kwa jina moja la Asha (20).

Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wamefika nyumbani kwa marehemu na kuzungumza na majirani wa familia hiyo ambao wamesema walikuta miili ya marehemu hao, ikiwa na kamba shingoni huku wakiwa wamewekwa nguo mdomoni.

“Baada ya jirani mmoja kuja kugonga kwenye hii nyumba na kukuta ukimya alilazimika kuchungulia ndani ndipo akamuona mama mwenye nyumba yupo chini amelala na ikaonekana miguu ya msichana wa kazi.

“Lakini yule mama alivyokuwa akionekana pale chini alionekana kama amekufa ikabidi atafutwe mwenyekiti wa serikali za mitaa akasema haiwezekani kuvunja mlango itabidi tuwatafute Polisi” amesema Halima Shebe ambaye ni jirani yake.

Shida huyo amebainisha kwamba baada ya polisi kufika walivunja mlango wa mbele na kuingia ndani akaonekana mama yuko kwenye korido wakaendelea mbele chumbani wakamkuta dada wa kazi naye amelala chini.

“Polisi walifanya taratibu zao za kutoa ile miili ya marehemu na kuiweka ndani ya gari, lakini mpaka sasa hatujui wale tukio wamefanyiwa na nani na baba mwenye nyumba mpaka saa izi anatafutwa hajulikani yuko wapi simu zake tangu jana hazipatikani kwahiyo hapa hatujui nani kafanya tukio hilo.

Jamhuri Digital inafanya taratibu za kuwasiliana na Kamaanda wa Polisi Mkoa wa Tanga ili kuzungumzia kwa kina tukio hili.

Please follow and like us:
Pin Share