Na Lookman Miraji

Tamasha la mitindo la kitanzania lijulikanalo kama Tanzania Fashion Festivals (TAFF) limechukua taswira taswira mpya mara baada ya kufanyika kwake mwishoni mwa wiki iliyopita.

Tamasha hilo lilifanyika jumamosi iliyopita ya septemba 28 mwaka huu katika ukumbi wa terrace ulioko masaki, Dar es Salaam.

Tamasha hilo limefanyika mwaka huu ukiwa ni msimu wake wa saba tangu lilipozinduliwa rasmi kwa mara ya kwanza mwaka 2018.

Kwa mwaka huu 2024 tamasha hilo lilihusisha wanamitindo wa kitanzania pamoja na wabunifu wa mavazi hapa nchini kuonyesha uwezo wao katika tasnia ya mitindo nchini.

Akizungumza na gazeti la Jamhuri digital, miongoni mwa watu walioshiriki kuandaa tamasha hilo ambae pia ni mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania Niller Benard amesema kuwa wanafarijika kuona ukuaji mkubwa na utofauti unaozidi kuonekana katika mfululizo wa tamasha hilo kila mwaka.

“Tumefurahi kuona kuwa kuna mabadiliko kila mara ukilinganisha na miaka ya nyuma. Kwa mwaka huu tumekuwa na mabadiliko makubwa kuanzia katika uchaguaji wa wanamitindo, wabunifu wa mavazi pamoja pia ubora wa mavazi yaliyotumika na wanamitindo “

Mwanamitindo huyo pia alisema kuwa pamoja na mabadiliko makubwa yaliyokuwepo katika tamasha hilo ila pia wametumia tamasha hilo kwaajili ya kulinda na kutangaza utamaduni wa kitanzania kwakuwa tamasha hilo linatambulika na serikali kupitia baraza la sanaa la taifa(Basata).

“Pia kumekuwa na muamko mkubwa kwa wabunifu wa mavazi kutumia fursa hii kujitangaza wao pamoja na kazi zao ambapo sisi kama waandaji tumekuwa tukisimamia ubora wa mavazi na kuhakikisha mavazi hayo yanalinda maadili ya mtanzania kwasababu tumukuwa tukitambuliwa na baraza la sanaa la taifa kwahivyo haya ni maonyesho ya mitindo lakini tunahakikisha pia tuko ndani ya maadili”

Aidha mwanamitindo huyo aliongeza kwa kuiomba serikali chini ya wizara husika ya utamaduni, sanaa na michezo kuipa nafasi fani ya mitindo kama ambavyo wamekuwa wakitoa nafasi kwa fani nyingine za sanaa ili kusaidia wanamitindo wakitanzania kufanya vizuri kimataifa. Miongoni mwa uwezeshwaji huo kutoka kwa serikali ni uendeshwaji wa mafunzo kwa wanamitindo ambao miongoni mwao wanauwezo mkubwa lakini wanakosa vitu vidogo vya kujikimu ili kulifikia soko la kimataifa.

“Kitu pekee ambacho ni kilio chetu ni kuona siku moja fani ya mitindo na urembo inapewa nafasi na serikali kama fani nyingine zikiwemo uigizaji na uimbaji. Kupitia tamasha hili tunaiomba serikali itupe nafasi kuona kama kuna namna yeyote ya kuendesha mafunzo kwa wanamitindo wetu ambao kati yao yanaonekana kuwa na vipawa vikuwa na uwezo lakini wanakosa uwezo kujikimu kwenda katika soko la kimataifa ” Alisema.

Kwa upande mwingine pia miongoni mwa makampuni yaliyoshiriki kama wadhamini katika tamasha hilo ni kampuni ya Jc decaux inayojishughulisha na mambo ya matangazo.

Akizungumza naye mwakilishi wa kampuni hiyo Ndg: Guremi Ikamba amesema kuwa kwao ni heshima kushiriki katika tamasha hilo ambapo wao kama taasisi kupitia mkakati wao maalumu uliolenga kuhusiana na mambo ya mazingira, jamii pamoja na mambo ya kiutawala hivyo wameona kupitia tamasha hilo la mitindo ni sehemu sahihi kwao kuwekeza nguvu zao kwani ni jambo linalohusiana na mambo ya kijamii ambapo ni miongoni mwa maeneo yaliyolengwa kushughulikiwa na kampuni hiyo.

“Kwetu sisi kama kampuni ni heshima kubwa kushiriki katika tamasha hili la mitindo ambalo tumekuwa tukishiriki mara kwa mara. Kupitia mkakati wetu tuliouweka ni kushughulika na maeneo baadhi ambayo ni mazingira, jamii pamoja na utawala hivyo tamasha hili limeanguakia katika upande wa kijamii ambapo kwetu sisi tumeona ni sehemu sahihi kushiriki kwani tumelitazama kwa namna ya utofauti mkubwa ikiwa tumeona lina mchango mkubwa katika kurudisha mchango kwa jamii yetu.”

“Tamasha hilo tumeona kuwa lina mchango mkubwa katika jamii kwani fani ya mitindo inahusisha watu kutoka nyanja mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara, wawekezaji na watu wa hali ya kawaida kimaisha hivyo kupitia tamasha inapatikana ile fursa ya kuunganisha mawazo ya watu na mwishowe kuzaliwa jambo lenye manufaa katika jamii” Alisema Ikamba.

Tamasha hilo kwa mwaka lilihusisha jumla wanamitindo zaidi ya 30 walioonyesha uwezo katika fani hiyo pamoja na wabunifu wa mavazi 24 ilijumuisha kampuni za mambo ya ubunifu wa mavazi zilizoshiriki kama wadhamini katika tamasha hilo.