Na Lookman Miraji, JamhuriMedia, Dar esSm Salaam

Viongozi wa vyama na mashirikisho ya michezo nchini wameaswa kuwasilisha hesabu za fedha kwa msajili ambapo ni kwa mujibu wa sheria zilizowekwa na baraza la michezo la taifa.

Akizungumza Septemba 30,2024 katika ofisi ya msajili wa baraza msajili mkuu wa baraza la michezo la taifa , Afisa msajili Ndg Evody Kyando ameeleza kuwa wanahimiza viongozi wa vyama kuwasilisha taarifa ya hesabu za fedha zilizoidhinishwa na wakaguzi kwa mujibu wa sheria.

Msajili huyo amesema kuwa kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizowekwa na baraza la michezo la taifa zinawataka viongozi wa vyama na mashirikisho kuwasilisha taarifa za fedha zilizoidhinishwa ikiwa lengo lake ni kuiwezesha serikali kujua upatikanaji wa fedha katika sekta husika, matumizi yake pamoja na mchango wake ni upi lakini pia kwenye upande wa masuala mazima ya utawala bora.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya tangazo rasmi lilitolewa mnamo agosti 13 mwaka huu na Baraza la Michezo la Taifa la kuvitaka vyama kuwasilisha taarifa za fedha kwa msajili wa baraza la michezo la taifa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa Agosti 13, 2024 ilivielekeza vyama kukamilisha mchakato huo kabla ya Agosti 31, mwaka huu.

Mpaka kufikia Septemba 30 ripoti iliyotolewa na msajili mkuu wa baraza la michezo la taifa inasema kuwa muitikio wake umekuwa mdogo ambapo jumla ya vyama vya michezo vilivyosajiliwa nchini vinatajwa kuwa kufikia idadi ya 13,392 .

Katika orodha ya vyama 13,392 mpaka sasa ni vyama 16 pekee ndivyo vimefanikiwa kuwasilisha ripoti hizo ambapo miongoni mwa vyama hivyo 16 vimeomba viongezewe muda ili viweze kukamilisha ripoti hizo.

Aidha kufuatia ripoti hiyo iliyotolewa leo Baraza la Michezo la taifa kupitia msajili limetangaza rasmi kuvichukulia hatua kali za kisheria vyama vyote vilivyokaidi maagizo hayo ambapo miongoni mwa hatua hizo ni kuvifutia usajili vyama na mashirikisho hayo endapo itakapothibitika kuwa havikutekeleza maagizo hayo pasipo sababu zozote za msingi.

Pia msajili Kyando ameeleza hatua hiyo ya kufutwa kwa mashirikisho mbali na kuhusisha vyama ambavyo havijawasilisha ripoti hizo pamoja na kulipa ada ya vyama itahusisha pia na wale ambao hawafanyi shughuli za michezo zilizoainishwa katika katiba zao ambapo orodha rasmi ya wahusika hao itatangazwa hivi karibuni.

Msajili Kyando alimaliza kwa kusema mpaka kufikia Oktoba 9, mwaka huu orodha hiyo ya vyama ambavyo vimekiuka maagizo hayo itakwenda kwa mamlaka zingine kwaajili ya kuwatangaza.

Please follow and like us:
Pin Share