Na Isri Mohamed

Mtoto Mtanzania Barka Seif ameandika rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka Ballon D’or of the Champions Dream nchini Hispania.

Barka anayekipiga kwenye Academy ya vijana ya CF Damm, ameshinda tuzo hiyo usiku wa kuamkia jana akiwashinda watoto wengine wa kimataifa waliokuwa wakiwania tuzo hiyo.

Barka amechangia kwa kiasi kikubwa timu yake kuchukua ubingwa wa Champions Dream kwa vijana chini ya umri wa miaka kumi, kwa kufunga mabao 10 na Asisti 8 za mabao.

Watu mbalimbali akiwemo Katibu mkuu wa wizara ya michezo, Sanaa na utamaduni, Gerson Msigwa wamempongeza Barka na kumtaka kuendelea kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania.

Kwa upande wake Barka amesema kushinda tuzo hiyo ni heshima kwake na kwa Tanzania nzima huku akiamini ndio chachu ya kuendelea kufanya vizuri katika safari yake ya kucheza soka.

Please follow and like us:
Pin Share