Na Aziza Nangwa

Mkurugenzi mlMkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU),Crispin Chalamila ,ametoa uzoefu wa namna ambavyo mfumo wa sheria na kitaasisi nchini Tanzania unaowezesha mapambano dhidi ya rushwa kufanikiwa.

Mkurugenzi huyo ameyasema hayo, wakati akiwasilisha mada kwenye kongamano la tano la kimataifa la mashirikiano katika mapambano dhidi ya rushwa.kuhusu ‘ANTI CORRUPTION AND INSTITUTIONAL LEGAL FRAME WORK IN TANZANIA’ kwa wakuu wa mamlaka za kuzuia na kupambana na rushwa wanaoshiriki ‘the 5th Global OPERATIONAL NETWORK OF ANTI CORRUPTION LAW ENFORCEMENT AUTHORITIES – GLOBE NETWORK’.

Amesema Serikali ya Tanzania imekuwa ikipambana na rushwa, kwa kuimarisha mifumo ya sheria na ya kitaasisi, ikiwemo kuanzishwa kwa divisheni ya mahakama kuu inayoshughulikia masuala ya rushwa na uhujumu uchumi.

Taaifa hiyo imedai kongamano hilo ni mahususi kwa ajili ya mamlaka za kuzuia na kupambana rushwa Duniani kubadilishana uzoefu na utaalamu katika jukumu la kuzuia na kupambana na rushwa.

Imedai pamoja na mambo mengine, kongamano hilo lilihusisha high level forum (warsha ya wakuu wa mamlaka za kuzuia na kupambana rushwa) kutoa uzoefu wao wa namna serikali zinavyofanikiwa kudhibiti rushwa katika mataifa yao.

Maeneo yaliyozungumziwa ni pamoja na 1. Global Vision,2. mfumo wa kisheria na kitaasisi,uendeshaji wa Globe Network na. kujenga ushirikiano

Kongamano hilo la siku tano linahudhuriwa na mamlaka 219 za kuzuia na kupambana na rushwa kutoka nchi 121 Duniani – Tanzania ikiwa ni kati ya nchi 70 zilizopewa fursa ya kutoa wasilisho.

Mtandao wa Globe ulianzishwa 2021 kwa lengo la kubadilishana taarifa, uzoefu na utaalamu katika mapambano dhidi ya rushwa na TAKUKURU ilijiunga na mtandao huu mwaka 2022.

Katika hatua nyingine, Chalamila, amemtembelea balozi wa Tanzania nchini China Khamis Mussa Omar kwa lengo la kujitambulisha.

Balozi Omar ameipongeza TAKUKURU, kwa jitihada inazozifanya katika kuzuia na kupambana na rushwa

Omary amesisitiza TAKUKURU kutumia vema fursa ya ushirikiano uliopo kati ya serikali ya Tanzania na ya China kwani kuna mambo mengi ya kujifunza.

Please follow and like us:
Pin Share