Na Cresensia Kapinga, JamhuriMedia, Tunduru

Rais Samia Suluhu Hassan amehutubia maelfu ya wananchi wa Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma akisisitiza umuhimu wa maendeleo ya jamii na ushirikiano katika kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo ya kuwaondoa Tembo kwa kutumia ndege nyuki kwenye makazi ya watu.

Alisema kuwa Serikali imekuwa ikifanyakazi kubwa ya kupeleka magari ya kufanya doria kwenye maeneo ya hifadhi pamoja na kununua ndege nyuki ambazo zinasaidia kufukuza Tembo maeneo ya mashambani na makazi ya watu.

Rais Samia ameyasema hayo jana wakati akihutubia wananchi wa Wilaya ya Tunduru katika mkutano wa adhara uliofanyika kwenye uwanja wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo.

Rais Samia Suluhu Hassan akizindua soko la madini wilayani Tunduru.

Amewaagiza viongozi wa mkoa huo kuhakikisha kuwa suala la Ndovu wanaovamia mashamba ya wananchi katika Wilaya za Namtumbo na Tunduru wanazishughulikia ili kuwawezesha wananchi kufanya shughuli zao ikiwemo kilimo wakiwa salama.

Aidha amewatoa hofu wananchi kuhusu changamoto ya uvamizi wa Ndovu kwa kuwahakikishia kuwa Serikali imechukuwa hatua stahiki kuhakikisha kuwa wanakuwa salama ikiwemo kuweka magari ya doria ,kutumia ndege nyuki (Drone) ilikuwakimbiza Ndovu na kuimarisha vituo vya askari.

Rais Dkt. Samia pia amezindua soko la madini wilayani humo lililojengwa kwa ubia kati ya wafanyabiashara wa wa madini na halmashauri hiyo.

Alisema kuwa Serikali inatambua mchango wa wachimbaji wadogo wa madini na inaendelea na mipango mbalimbali ya kuwainua ikiwemo mitambo ya kuchoronga madini.

Kwa upande wao wabunge wa Jimbo la Tunduru Daimu Mpakate na Hassan Kungu walimwekeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kero ya Ndovu na mifugo aina ya ng’ombe ambao wamekuwa akivamia mashamba ya wananchi na kula mzao yao.

Wananchi wa Tunduru wakiwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa CCM wilayani humo.

Mbunge Daimu Mpakate alisema kuwa vijiji 14 wamavamiwa na Ndovu ambao wamekula mazao ya wakulima jambo ambalo limesababisha wakulima hao kuwa maskini.

Aidha wamemshikuru Rais kwa upande wa miradi ya maendeleo ambayo amewaletea fedha kwenye sekta ya elimu, afya, maji, miundombinu ya barabara na madaraja lakini pia kwenye upande wa nishati ambapo vijiji vyote vya halmashauri hiyo vina umeme.
Mwisho.

Please follow and like us:
Pin Share