Na Cresensia Kapinga, JamhuriMedia, Mbinga

Rais  wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  Dk.Samia Suluhu  Hassan  ameridhishwa na ujenzi wa Jengo la kisasa la ghorofa moja la Halmashauri ya wilaya ya  Mbinga  ambalo limejengwa kwa shilingi bilioni 3.3 hadi kukamilika kwake.

Alisema kuwa anawashukuru amefika Mbinga kwa madhumuni ya kufungua jengo na amewapongeza halmashauri hiyo kwa kukamilisha ujenzi huu wa jengo hilo zuri .

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan hayo ameyasema wakati akifungua jengo la ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Mbinga mkoani Ruvuma.

Akizundua jengo hilo Septemba  25/2025 amesema kukamilika kwa jengo hilo ni kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) baada ya kukamilika jengo hilo wahakikishie huduma zote zinatolewa ndani ya nyumba moja .

“Ni jengo zuri nimeingia ndani kuangalia ujenzi unaridhisha sana na ni jengo lenye nafasi za kutosha kwa hiyo nawashukuru sana lakini pamoja na hilo niwapongeze madiwani kwamba mmesimamia ujenzi wa jengo hili lakini pia mmewaza kuwa na jengo la kitega uchumi jengo la kuwawezesha wananchi nimuombe Mungu awatie nguvu na mlimalize jengo hilo liweze kufanya kazi iliyokusudiwa” alisema Rais Samia.

Alisema kuwa kukamilika kwa jengo hilo ni kukuwa kwa utawala bora maofisi yote wakiwemo wakuu wa idara na kila mtu yumo humo ndani kwa maana hiyo huduma zote zitatolewa ndani ya nyumba moja ili kuharakisha huduma kwa wananchi lakini pia kuleta utawala bora ili haki za wananchi zinashughulikiwa haraka iwezekanavyo .

” Niwasisitize watakaotumia nyumba hii madhumuni ya serikali kujenga nyumba hizi ni kuleta mazingira mazuri kwa maafisa wetu wanafanya kazi ndani ya halmashauri hizi ni kurahisisha utendaji wa kazi kwa hiyo niwaombe sana maofisa wote kutumika Majengo haya kwa kutulia na kufanya kazi zao vizuri kwa kuhudumia wanachi kwa upendo na weledizaidi.”alisema Rais Samia.

Naye Mbunge jimbo la Mbinga Vijijini  Benaya Kapinga amesema,Wanamshukuru kwa miradi mingi aliyopeleka kwenye jimbo hilo wamepata miradi ya maji bilioni 13.9 , Barabara-Amani Makolo-Mbambabay bilioni 60 elimu bilioni 10 afya bilioni 2.2 ujenzi wa vituo vya  Afya bilioni 836  na bilioni 2.8 upande wa Barabara.

Alisema kuwa pamoja na fedha zote za miradi yote ya maendeleo waliyopata anakabiliwa na changamoto  mbalimbali ikiwemo Mji huo wa Kiamili  unakua kwa kasi jambo ambalo linasababisha huduma ya maji  hayatosherezi.

Madini ya makaa ya Mawe wananchi hawakunufaika ila sasa wameanza kupata CSR ila bado wanamang’uniko makampuni yanapata pesa nyingi kuliko CSR inayopelekwa.Kahawa bila Ruzuku ya  mbolea hawavuni .Changamoto  ipo bado hawana maghala ya kuhifadhi mazao  yao ila bado Kuna msululu mkubwa mtaaani 350 kwa kilo .

Kahawa haijauzwa chini ya 4000 mwaka huu kilo imeuzwa 10,000 hadi 12,000 kwa kilo .

Barabara  amani Makoto hadi Ruanda  desemba  18 , 2023 ila bado haujakamilika hadi leo kipande cha kwanza km 35 bado hakijakamilika wala kipande cha pili km 56  hakijakamilika.

Naye Mbunge wa Viti maalum kupitia vijana Judith Kapinga na Naibu Waziri  Nishati  amemshukuru  Rais Samia Suluhu na amemuomba   awasaidie kuweka kituo cha Zana za kilimo ili wakulima waweze kuzalisha kwa wingi mazao yao.

Waziri wa Tamisemi Mohamed Mchengelwa amemshukuru Rais kwa kuwajengea Jengo zuri  lililogharimu  sh 3.3 bilioni wananchi hivyo kusogeza huduma kwa wananchi kwani wameteseka kwa muda mrefu kutafuta huduma za kijamii, ametoa sh 500 milioni kwa ajili ya ujenzi wa shule tatu za kata fedha zifike mara moja  kujenga shule hizo.

Naye Waziri wa kilimo Hussein Bashe amesema kuwa Bilioni 10 zimeshalipwa kwa wakulima  kuanzia mwaka kesho vituo vyote vya NFRA vitakuwa na mashine za kusafisha mahindi hivyo hakutakuwa na mateso

Mbegu za Ruzuku zitaanza kutolewana amewataka wakulima kutowauzia  madalali mahindi adala yake wapeleke mahindi kitengo Cha Taifa Cha hifadhi ya chakula (NFRA) na amewataka  wasiuze yote ili wale wa Dar es salaam bustani zao wapande Mahindi.

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa Rais anaenda kuzindua Barabara ya Mbinga -Mbambabay  kufunguka kwa barabara hiyo kunaenda kuhamsha Ruanda-Ndumbi pia wamepata mkandarasi hivyo kazi itaendelea.

Lukuyufusi -Mkenda kuelekea Msumbiji  itaanza kujengwa na kwenda kumaliza changamoto hizo.

Please follow and like us:
Pin Share