Na Isri Mohamed

Wakati akisubiri kusikiliza kesi yake katika kituo cha Metropolitan Detention Center cha Brooklyn, New York City, Rapa Sean Didy Combs maarufu kama P Didy, ameomba kuzungumza na watoto wake kwa njia ya simu ili kujua hali zao.

Diddy, (54) ambaye anakabiliwa na mashtaka ya unyanyasaji wa ngono na ulaghai, ana jumla ya watoto saba kwa wanawake wanne tofauti, ambapo ni Quincy (33), Justin (30) Christian (26) Chance (18), Jessie na D’Lila, (17), na wa mwisho ni Love mwenye miezi 23.

Didy ameomba kuzungumza na watoto wake ili kuwashusha presha kwani wanadaiwa Watoto kuwa katika taharuki na mshtuko kufuatia kukamatwa kwa baba yao.

Diddy alikamatwa na kushtakiwa wiki iliyopita kwa biashara ya ngono, ulaghai na usafirishaji wa binadamu wanaojihusisha na ukahaba.

Shtaka hilo, ambalo linaelezea madai ya mwaka 2008, linamtuhumu Didy kwa kuwadhulumu, kuwatishia na kuwalazimisha wanawake kwa miaka mingi ili kutimiza tamaa zake za ngono, kulinda heshima yake, na kuficha mienendo yake, ambapo amekana mashtaka yake yote.

Please follow and like us:
Pin Share