Na Cresensia Kapinga, JanhutiMedia, Songea

RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan,amewataka Watanzania kuendelea kudumisha mila na Desturi za Kitanzania,badala ya kuiga utamaduni wa Mataifa ya nje yanayochangia mmonyoko wa maadili kwa vijana hapa nchini.

Rais Samia amesema hayo leo wakati akifunga Tamasha la Tatu la Kitaifa la Utamaduni lililofanyika katika uwanja wa michezo wa Majimaji katika Manispaa ya Songea.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa Manispaa ya Songea.

Alisema kuwa wananchi wanapaswa kuenzi na kutunza mila na desturi zao na kwamba utamaduni ni nguzo muhimu ya Taifa na matamasha hayo yanasaidia kuleta pamoja wanajamii ,kuonesha talanta na ubunifu wa vijana kwa kuvutia watalii.

“Tamasha hili la tatu la utamaduni mkoani Ruvuma lilete umoja na maendeleo ya kitaifa na kuimarisha mshikamano kati ya jamii tofauti nchini.” alisema.

Alisema kuwa tamasha hilo ni kielelezo cha namna tunavyothamini na kuenzi tamaduni zetu na mkusanyiko huu ni kielelezo cha uwahi wa tamaduni zetu zilizowekwa na wazee wetu kwani tumekusanyika kutoka kila pembe ya nchi yetu .

Rais Samia alisema kuwa Tamasha hilo limefungua fursa za kiuchumi kwa Watanzania kupitia kazi za sanaa ,utamaduni kwani tunaposema utamani ni pamoja na vyakula vyetu .

“Nilipofika hapa nilipitishwa kwenye maonesho na katika banda la Mkoa wa Ruvuma nimesoma kila utamaduni wa Ruvuma ndani ya banda lile ,vyakula,mavazi yaliyokuwepo yakitumika zamani laini kwa sasa tumeiga tamaduni za kizungu kwa hiyo nawapongeza sana kwa kuendeleza mambo hayo “.alisema Rais Samia.

“Niwape moyo Watanzania wenzangu wakiwemo wdau wa sekta ya utalii kwa namna ya kuufanya utamaduni wetu kuwa biashara iliutuletee manufaa ya kiuchumi nataka niseme nimezunguka mabanda ya maonesho na nimefurahishwa sana na banda la Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa namna wanavyofanya mabadiliko ya sera na kuufanya utamaduni ,Sanaa na ubunifu sasa kuwa ni ajira na biasharana uchumi ,nawasii BASATA msimamie vizuri.”alisema Dkt. Samia.

Ameagiza matamasha yajayo yawe na msukumo mkubwa kwa kushirikisha sekta nyingi binafsi ,tamasha kama hilo likitangzwa vyema linakuwa ni jambo kubwa sana na mikoa itakuwa inagombania kuwa wenyeji wa matamasha hayo kwa kuwa nifursa kubwa kiuchumi kwa jamii.

Hata hivyo Rais Samia amewataka wafanyabiashara mkoani humo kuona umuhimu wa kuwekeza kwenye sekta ya Hotel pamoja na nyumba za kulala wageni ili kushawishi watu wengi zaidi kufika Ruvuma kufanya Matamasha mengine ambayo yameonekana kuwa na fursa nyingi kwa jamii.

Aidha amefafanua kuwa pamoja na kufunga tamasha hilo atafanya ziara ya siku sita mkoani humo ambapo atatembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya,maji,elimu na Miundombinu ya barabara iliyotekelezwa kwa fedha nyingi zilizotolewa na serikali.

Awali waziri wa utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro alisema kuwa lengo kuu la tamasha hilo ni kutoa fursa kwa watanzania kuhufamu vyema utamaduni wetu ,mila ,Desturi,historia yetu ,miiko pamoja na kuusherekea utamaduni wetu kwa kuuthamini na kuendeza .

“Hapa jambo la msingi ni kwamba ni wajibu wetu kuutetea ,kuulindana kuendeleza urithi wa utamaduni ambao tumeurithi kutoka kwa mababu zetu ,tupo hivi tulivyo kutokana na utamaduni wetu”alisema Dkt. Ndumbaro.

Pia Waziri Ndumbaro ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Songea mjini alisema Tamasha la Taifa ia utamaduni linaleta pamoja watu wa makabila mbalimbali kutoka kila kona Tanzania kuweza kusherehekea uhai wa urithi wa utamaduni wa kukaa pamoja kama ndugu.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahamed Abas Ahamed ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa pembejeo za kilimo za ruzuku kwa wakulima kwa bei nafuu hali iliyowawezesha wakulima kufanya shughuli zao za kilimo bila wasiwasi wowote na kwamba soko la mahindi kwa wakulima limekuwa zuri kutokana na bei nzuri.

Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Damasi Ndumbaro akimkaribisha mgeni rasmi Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan Jana kwenye kufungwa Tamasha la utamaduni la Kitaifa mkoani Ruvuma
Katibu Mkuu Wizara ya utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa akitambulisha wageni.
Please follow and like us:
Pin Share