Na Tatu Mohamed, JamhuriMedia, Dar es Salaam

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema kuwa linawashikilia watu 14 kutokana na kujihusisha na maandamano.

Limewataja baadhi ya watu hao ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Taifa (Chadema) Freeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti Chadema Bara, Tundu Lissu na Mwenyekiti wa chama hicho kanda ya kaskazini, Godbless lema.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 23, 2024 Kamanda Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema wamewakamata kwa kuwakaidi amri halali ya polisi ya kuacha kushiriki maandamano.

“Jeshi la polisi lilifuatilia kwa ukaribu matamko mbalimbali ya viongozi wa chama kile ya kuhamasisha maandamano hayo, kufuatia matamko hayo Jeshi Polisi lilipiga marufuku na kutoa katazo kwamba yasifanyike lakini waliendelea kutoa matamko.

“Kwahiyo leo hii tumewakamata watuhumiwa hawa ambao walikaidi kwasababu ambazo tulizieleza na mahojiano yanaendelea,” amesema Muliro.

Please follow and like us:
Pin Share