Isri Mohamed

Wachezaji wa klabu ya Simba leo alfajiri Agosti 11, wameondoka nchini kuelekea Libya kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika watakaocheza dhidi ya klabu ya Ahly Tripoli ya nchini humo.

Katika mchezo huo utakaochezwa Septemba 15, katika dimba la Tripoli Stadium, Simba ana kibarua kizito cha kupata ushindi ugenini dhidi ya timu yenye mafanikio na uwekezaji mkubwa.

Ahly Tripoli ni klabu ya pili kwa mafanikio nchini Libya ikiwa na mataji ya ligi kuu 13, lakini ndio klabu yenye mafanikio zaidi kimataifa nchini kwao.

Mafanikio yao makubwa waliyoyapata ni kucheza nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Afrika mwaka 2022 na Robo fainali ligi ya mabingwa Afrika 2017.

Msimu uliopita walimaliza nafasi ya tatu kwenye ligi kuu yao, ambapo kufuatia kutoridhishwa na matokeo hayo, wakazama mfukoni na kufanya usajili mkubwa wenye uwezo wa kurejesha heshima yao.

Miongoni mwa usajili wa kushtua waliofanya ni wa mshambuliaji Mabolulu ambae amesajiliwa kwa dau la Bilioni 4 na inatajwa kuwa ndio usajili mkubwa zaidi katika historia ya klabu hiyo.

Mechi ya pili ya marudiano ni Septemba 22, katika Simba la Benjamin Mkapa.

Please follow and like us:
Pin Share