Na Tatu Mohamed, JamhuriMedia, Dar es Salaam

TAASISI ya Internet Society Tanzania Chapter(ISOC-TZ) kupitia jukwaa la usimamizi wa mtandao Tanzania Internet Governance Forum(TzIGF) imeendesha mafunzo kwa vijana kuwajengea uwezo katika masuala ya usimamizi wa mitandao.

Akizungumza katika Mafunzo hayo yaliyofanyika leo Septemba 4, Jijini Dar es Salaam, Rais wa ISOC -Tz Nazar Kirama amesema kuwa vijana ndio viongozi wa baadae hivyo wanahitaji kujengewa uwezo katika masuala ya usimamizi wa mitandao.

Rais wa ISOC – Tz, Nazar Kirama akizungumza na washiriki ambao ni vijana kutoka vyuo vikuu pamoja na taasisi mbalimbali zinajishughulisha na masuala ya kimtandao katika mafunzo waliyoyaandaa kupitia jukwaa la usimamizi wa mtandao Tanzania Internet Governance Forum(TzIGF).

Amesema vijana wana nguvu ya kushawishi serikali kuweka usawa wa matumizi ya internet vijijini na mjini pamoja na kushauri gharama za vifurushi kushuka ili kila mtanzania aweze kupapta huduma za mawasiliano hayo.

“Kwahiyo tukaamua kufanya Mafunzo haya, tukiamini kuwa vijana wakijengewa uwezo katika usimamizi wa mitandao ndio daraja la kufanya kuwepo usawa wa matumizi kutokana vijana kuwepo katika sehemu za maamuzi na kufanya kurahisisha michakato yake,” amesema Kirama.

Amebainisha kuwa katika upatikanaji wa huduma za mtandao baadhi ya maeneo hawapati kwa ubora ambapo jukumu la vijana hao wanawajibu kushauri watunga sera juu ya kupata uwiano.

Naye Janeth Kahindi kutoka Taasisi ya TECH and Media Convergency (TMC), amesema mafunzo ni muhimu kwani Dunia ipo katika ulimwengu wa kidigitali hivyo itasaidia vijana kufahamu haki za kimtandao, mipaka pamoja na sheria.

“Ni muhimu zaidi kwa vijana kujifunza masuala haya kwasababu wengi wao wanatumia internet katika mambo mbalimbali ikiwemo kutengeneza ajira na pia vijana ni kizazi cha kesho itasaidia kuwa na kizazi salama.

“Nitoe wito kwa wadau wengine kuendelea kutoa mafunzo kama haya lakini pia niwashauri vijana wenzangu kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza katika kujifunza kuhusu masuala mazima ya kimtandao kwani kwa sasa yana nafasi kubwa katika jamii,” amesema Janeth.

Kwa upande wake, Cyidion Cylivanus kutoka Chuo cha Mipango, amewashukuru ISOC kwa mafunzo hayo, ambapo amesema matumizi ya intaneti yanakuwa kwa kasi hivyo yanapaswa kuwa na faida kwa vijana na sio anasa.

“Gharama ya intaneti zikiwa kubwa vijana hawataweza kuitumia katika kuwaingizia kipato badala yake matumizi hayo yatageuka kuwa anasa kufanya vijana kuwa nje,” amesema Cylivanus.

Amesema kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya intaneti kwenye dunia ya teknolojia kwa vijana wanatakiwa kuchechemua katika maeneo ya utoaji wa elimu kuhusiana na matumizi sahihi ya mtandano yasiyoacha madhara baada ya kutumia.

Thadei Mkanzabi kutoka Taasisi ya Digital Opportunity Trust (Dot) akiwasilisha mada wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa Taasisi ya Internet Society Tanzania Chapter (ISOC-TZ) kupitia jukwaa la usimamizi wa mtandao Tanzania Internet Governance Forum(TzIGF)
Please follow and like us:
Pin Share