Na Isri Mohamed, JamhuriMedia, Dar es Salaam

KLABU ya Azam FC leo Septemba 03, imetangaza kuwafungashia virago Kocha wao Mkuu, Youssouph Dabo na wasaidizi wake wa benchi la ufundi aliokuja nao kufuatia matokeo mabaya ya timu.

Azam FC chini ya Kocha Dabo aliyehudumu kwa kipindi cha mwaka mmoja, imeshiriki michuano ya kimataifa na kutolewa hatua ya awali tu, ambapo msimu huu imetolewa na APR ya Rwanda.

Kwa upande wa Ligi Kuu msimu huu Azam FC imeanza kwa kupata matokeo yasiyoridhisha kwa kuambulia alama moja tu dhidi ya JKT Tanzania.

Bodi ya Azam FC ipo kwenye mchakato wa kutafuta kocha mpya, kipindi hiki programu za timu zitakuwa chini ya makocha wa timu za vijana.

Please follow and like us:
Pin Share