Na Isri Mohamed, JamhuriMedia, Dar es Salaam

ALIYEKUWA beki wa Simba msimu uliopita, Israel Patrick Mwenda, ambaye msimu huu amesajiliwa na klabu ya Singida Black Stars ameibuka na kudai kuwa kwa sasa hana timu licha ya kudaiwa kupokea ada ya usajili Milioni 140 za Singida.

Mwenda amezua gumzo mitandaoni baada ya Singida kutoa taarifa ya kusikitishwa na kitendo chake cha kutoripoti kambini licha ya kumtimizia matakwa yote ya kimkataba, ambapo anawadai Milioni 60 tu ambazo wangemlipa taratibu ndani ya muda wa mkataba.

“Nipo kwenye mchakato wa kuvunja mkataba, nyie subirini mtapata taarifa, Singida wapo nje ya makubaliano tuliyokubaliana, Mpira wetu una changamoto sana, Halafu baadae utasikia wazawa wana matatizo”

“Nitaenda wapi sababu dirisha limefungwa? Hela niliyonayo inanitosha kuishi hata misimu minne bila kucheza mpira, kiufupi ni kwamba sina timu” amesema Mwenda.

Aidha Mwenda amekanusha taarifa ya kupata timu mpya kuwa ndio sababu ya kutoripoti kambini na badala yake amewataka watanzania kuvuta subra katika kipindi hiki ambacho suala lake linashughulikiwa kisheria.

Please follow and like us:
Pin Share