Na Magrethy Katengu,JamuhuriMedia,
Dar es Salaam

Waziri Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tamisemi Mohamed Mchengerwa amewataka Watendaji wa mabasi yaendayo haraka DART kuhakikisha wanafanya mchakato wa haraka kupunguza changamoto ya usafiri inayosababishwa na uhaba wa mabasi hayo .

Agizo hilo amelitoa Septemba 2, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa mfumo wa matumizi ya kadi janja ambapo amesema licha ya kuwa na mfumo huo ambao unakwenda kuondoa matumizi ya karatasi lakini ni budi DART kushirikiana hata na kampuni binafsi za usafiri ili kuleta suluhisho la changamoto ya abiria kukaa zaidi ya masaa kusubiria usafiria huo .

” Mimi nimekuwa nikipokea malalamiko mengi kuhusu usafiri huu wa mwendokasi kuwa watu wanakaa vituoni muda mrefu kusubiria usafiri na nikiomba majibu kwa nini kuna changamoto hiyo naambiwa michakato inafanyika ni muda mrefu sasa barabara ya Mbagala imeisha na mabasi hakuna hivyo nawasihi angalieni suala hili kwa jicho la tatu” amesema Waziri.

Sanjari na hayo amewaagiza watu wa tehama kuwa kadi hizo zinapatikana kwa urahisi na mfumo usilete shida kabisa na kuanza kulalamikiwa na wananchi wakati Rais Dk Samia Suluhu alitoa fedha wakapatiwe mafunzo namna ya kuundesha .

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mabasi yaendayo haraka DART , Othmani Kihamia amebainisha mfumo huo unakwenda kuanza kutumika mara moja baada ya uzinduzi huo na utapunguza foleni , usumbufu wa chenji na matumizi ya karatasi .

Please follow and like us:
Pin Share