Na Aziza Nangwa,JamhuriMedia, Dar es Salaam

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) ,limetoa tahadhali kwa wananchi na wadau juu ya uwepo wa upepo mkali kwa siku tatu kwenye baadhi ya maeneo kwenye ukanda wa Pwani,ya kusini mwa Bahari ya Hindi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya Mkurugenzi mkuu wa TASAC imesema ni vyema wadau wanaotumia usafiri kwa njia njia ya bahari na wanaofanya shughuli za kiuchumi kwenye maziwa kutokana na kuwepo kwa upepo mkali kwa siku tatu mfululizo kuanzia jana hadi kesho.

TASAC imetoa taadhali hiyo baada ya kupokea taarifa ya upepo huo kutoka kwa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), juu ya uwezekano wa kuwepo kwa upepo mkali unaozidi kilomita 40 kuanzia Septemba 1 hadi 3.

Taarifa hiyo imeeleza maeneo yatakayoathirika ni pamoja na ukanda wa
Pwani ya kusini mwa Bahari ya Hindi ,ikiwemo Mikoa ya Lindi na Mtwara na maeneo mengine ya kusini mwa ziwa Tanganyika hasa Mikoa ya Rukwa na Katavi.

Aidha limewalekeza wadau wote wanaofanya shughuli za kiuchumi kwa njia ya maji ,kama vile wavuvi pamoja na wasafiri shaji wadogo
kufuatilia taarifa za hali ya hewa kutoka TMA ili kuepuka madhara yatokanayo na upepo huo.

Pia taarifa hiyo imewataka wadau hao kuwasiliana na kituo cha kuratibu shughuli za utafutaji na uokoaji majini, pindi inapotokea
dharula mpaka hapo itakapo tangaza hali ya hewa kuwa shwari ili kuzuia ajali zitakazo hatarisha maisha ya wavuvi na wasafiri

Please follow and like us:
Pin Share