Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia,Manyara

TUME huru ya Taifa ya Uchaguzi imewataka watendaji Mkoa wa Manyara kutumia elimu na ujuzi walioupata kwenye mafunzo ya uandikishaji wa zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Akizungumza katika mafunzo kwa watendaji hao Jaji wa Mahakama kuu Tanzania, Asina Omar amesema watendaji hao wanapaswa kufanya kazi kwa weledi na moyo wa kujituma pamoja na kutumia uzoefu walionao ikiwemo Elimu waliyoipata ili kukamilisha zoezi hilo.

“Matarajio ya tume Kutokana na mafunzo haya kila mmoja wenu atapata elimu na ujuzi wa kutosha utakaowezesha kutekeleza majukumu yake ili kufanikisha uboreshaji wa daftari,mafunzo haya yatahusisha namna ya ujazaji wa fomu pamoja na kutumia mfumo wa kujiandikisha wapiga kura”.

Aidha,amesema wakati wa uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura mawakala na viongozi wa vyama vya siasa hawaruhusiwi kuingilia mchakato wa uboreshaji wa daftari la mpiga kura hapo kituoni.

Mkaguzi Afisa wa Uhamiaji Mkoa wa Manyara, Castor Makungu amesema waandikishaji wanapaswa kuwa makini katika zoezi la uandikishaji na kuchukua taarifa muhimu kutoka kwa raia huku wakipaswa kutoa taarifa kwa Jeshi la uhamiaji endapo wakipata wasiwasi wa muadikishwaji.

Please follow and like us:
Pin Share