Na Isri Mohamed, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Kaimu kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Hemed Suleiman ‘Morocco’ ametoa ufafanuzi kuhusu kukosekana kwa washambuliaji Mbwana Samatta na Simon Msuva, kwenye kikosi cha Stars kilichoitwa leo kwa ajili ya kujiandaa na michezo miwili ya kufuzu AFCON 2025 dhidi ya Ethiopia na Guinea.

“Samatta bado ni mchezaji wa timu ya taifa na tunachagua wachezaji kulingana na mechi na wapinzani tunaoenda kucheza nao na hata tulipocheza na Zambia hakuwepo lakini bado ni mchezaji wa timu ya taifa na nimeongea nae kwa muda mrefu na tumefika sehemu nzuri.!”

“Kulikuwa na changamoto mbili tatu lakini tumeshaweka sawa. Niwaondoe wasiwasi, Samatta yupo na tukimuhitaji atakuja tu.”

Aidha Kocha Morocco ameelezea Kuhusu Simon Msuva.

“bado ni mchezaji wa timu ya taifa nimeongea nae na sasa hivi anafuatilia masuala yake ya kujiunga na timu anayotaka kujiunga na ni mchezaji ambaye tunamuhitaji sana katika timu na lakini kama hana timu ya kucheza inakua changamoto.”

“Atakapopata timu ya kucheza na akawa na mwendelezo mzuri, tukiangalia perfomance yake anaweza akaja kutusaidia.”

“Ni vigumu kumuita mchezaji timu ya taifa wakati bado anafikiria masuala ya yake ya mikataba na timu mpya, Tutamuita kwenye michezo ijayo inayofuata.” – amesema kocha Hemed Suleiman Morocco

Please follow and like us:
Pin Share