Kundi la Hezbollah limesema kwamba limerusha makombora zaidi ya 320 kuelekea Israel alfajiri ya Jumapili.

Katika taarifa iliyotolewa mapema Asubuhi, kundi hilo lilisema kwamba lililenga maeneo kumi na moja ya kijeshi kaskazini mwa Israel kwa kutumia maroketi za aina ya Katyusha.

Ni awamu ya kwanza ya shambulizi hilo dhidi ya Israel ambalo limekamilika, lilisema kundi hilo.

Aidha limeendelea kusema kwamba awamu ya kwanza ililenga kambi za kihsei za Israel huku Hezbollah ikisema kwamba itatoa taarifa zaidi baadaye.

Please follow and like us:
Pin Share